Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Mlinzi Aliyempiga Aliyekuwa Akimuuguza Mgonjwa Achukuliwa Hatua


Meneja wa Kampuni ya Ulinzi ya Suma JKT Guard Kanda ya Ziwa, Captain Manika Kihiri amesema baada ya kutokea tukio la Mlinzi wake kumshambulia Daudi Hospitali ya Rufaa Shinyanga, hatua za awali walizochukua ni kumuondoa Mlinzi huyo eneo la Hospitalini na watatekeleza maagizo yaliyotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua za kinidhamu kwani Suma JKT haipo kwa ajili ya kuzua taharuki bali kuleta amani.


Tukio hilo limetokea Ijumaa Januari 22,2020 saa 11 jioni ambapo Daudi Lefi (45) akiwa katika wodi ya Wanawake namba 1 ambako Mama yake mzazi Victoria Lugano Mwakagari amelazwa, alishambuliwa kwa kupigwa mkanda sehemu mbalimbali za mwili wake na Mlinzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga kutoka Kampuni ya Ulinzi ya Suma JKT Guard Geofrey Paul akimtaka aondoke wodini kwakuwa muda wa kusalimia Wagonjwa umeisha.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments