Rapper T.I na Mkewe Watuhumiwa Kufanya Vitendo vya Ukatili kwa Wanawake 25

advertise here

 


Wanawake zaidi ya 25 wamejitokeza na kudai kuwahi kufanyiwa vitendo vya kikatili na T.I. pamoja na mkewe Tiny Harris.


Wanawake hao wamejitokeza kupitia ukurasa wa mwanadada Sabrina Peterson ambaye wiki hii aliibuka kupitia Instagram na kudai T.I. aliwahi kumtishia bastola. Baadaye rapa huyo pamoja na mkewe waliibuka na kupinga tuhuma hizo za Sabrina.


Kuonesha kwamba Sabrina alidhamiria kuonesha maovu ya T.I. ambaye jamii inamkumbatia kama mfano wa kuigwa, alianzisha kampeni ya kuwakaribisha instagram Wanawake wote ambao waliwahi kufanyiwa vitendo vya kikatili na rapa huyo wa Marekani pamoja na mkewe.


Kwenye maelezo yao, wote wanadai kuwa T.I. na mkewe wanafanya biashara haramu ya kusafirisha binadamu na kuwatumia kingono (Sex Trafficking) ambapo kwa pamoja huwalewesha kwa dawa za kulevya na kufanya mapenzi kwa nguvu.


Wawili hao bado hawajazungumza chochote kuhusu madai ya Wanawake hao ambao wanaendelea kuongezeka kutoa ushahidi.

 

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE