Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Virusi vya corona: Rwanda, Burundi, UAE nazo zawekewa marufuku kuingia Uingereza


Rwanda,Burundi na Umoja wa falme za kiarabu zimeongezwa kwenye orodha ya nchi zilizowekewa marufuku ya kuingia nchini Uingereza.

Rwanda na Burundi zinajiunga na Tanzania, Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Afrika Kusini ambazo pia zimewekewa marufuku hiyo na Uingereza.


Hatua hiyo inalenga kudhibiti kuenea kwa aina mpya ya kirusi cha Afrika Kusini, na marufuku hiyo inaanza kufanya kazi siku ya Ijumaa saa saba kwa saa za Uingereza


Raia wa Uingereza, Ireland na raia wenye haki ya makazi nchini Uingereza wataruhusiwa kuingia lakini kwa sharti la kujitenga kwa siku 10 wakiwa nyumbani


Watu wenye ushawishi kwenye mitandao ya kijamii walitembelea Dubai majuma ya hivi karibun ,pamoja na kuwepo marufuku ya kusafiri iwapo hakuna ulazima wa kusafiri.


Walisisitiza kuwa safari zao ni kwa ajili ya kazi, lakini idara ya usafiri imesem misamaha yoyote ya kusafiri ambayo kawaida ipo haitakuwepo, ikiwemo kusafiri kwa sababu za kibiashara.


Pia safari za moja kwa moja za ndege za abiria kutoka Uingereza kwenda Umoja wa falme za kiarabu zitapigwa marufuku.


Kwa nyongeza ya nchi hizo inamaanisha kuwa nchi 33 zimewekewa marufuku hiyo mpaka sasa.


Waziri wa usafiri Grant Shapps amesema abiria wanaoruhusiwa kuingia Uingereza watahitaji uthibitisho kuwa hawana maambukizi ya virusi vya corona kabla ya kuwasili, vinginevyo watapigwa faini ya pauni 500.


Uwanja wa ndege wa Dubai umesema kuwa ndege za moja kwa moja zinazotarajiwa kuwasili Uingereza baada ya saa saba, saa za Uingereza zimeahirishwa na umewaambia abiria waliokuwa wakitarajia kusafiri wasiende uwanja wa ndege.


Shirika la ndege la Etihad pia limesema ndege zake zq abiria wake wanaokwenda Uingereza zitaahirishwa mpaka maelekezo mengine yatakapotolewa na wanafanya mipango na wateja wao kuhusu mipango ya kusafiri.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments