2/20/2021

Amuua Mama’ake Mzazi kwa Kumkata Shingoni Kisa UtajiriJeshi la polisi mkoani Kagera linamshikilia Fredius Philibart Kibengo mkazi wa Omurushaka wilayani Karagwe kwa tuhuma za kumuua mama yeke mzazi kwa kumkata shingoni kwa kutumia kitu chenye ncha kali baada ya mganga wa kienyeji kumtaka kupeleka damu ya mama yake. au ndugu yake wa karibu ili kutengenezewa dawa za kuongeza utajiri kwenye biashara.

 

 

Katika uchunguzi uliofanywa na jeshi la polisi mkoani Kagera umebaini kuwa katika kipindi cha siku chache kabla ya tukio hilo kutokea mtuhumiwa alisafiri kuelekea nchini Burundi kutafuta dawa za kuongeza utajiri na aliporejea nyumbani kwake alimshirikisha mkewe kuhusu mashariti aliyopewa na waganga wa kienyeji lakini mke wake hakukubaliana na masharti hayo.

 

 

Hata hivyo Februari 17 mwaka huu mtuhumiwa alionekana maeneo ya nyumbani kwa mama yake mzazi na ilipofika usiku wa kuamkia Februari 18 alimvamia mama yake na kumkata na kitu chenye ncha kali kisha kupoteza maisha.

 

 

Hata hivyo kamanda malimi amewataka wakazi wa mkoa wa kagera kujiepusha na imani za kishirikina ambazo zimekuwa zikichangia mauwaji ya wananchi wasio na hatia.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger