2/03/2021

Bilionea Jeff Bezos Ajiuzulu Kuwa Mkurugenzi wa Kampuni yake ya Amazon

 


Mwanzilishi wa kampuni ya Amazon Jeff Bezos amejiuzulu katika wadhifa wake wa mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo ya biashara ya mtandaoni ambayo ilianza katika gereji yake karibu miaka 30 iliyopita.

Bwana Bezos sasa hivi atakuwa mwenyekiti, hatua aliyosema itampa "muda na nguvu zaidi" kuangazia biashara zake zingine.


Nafasi ya Bwana Bezos, ambaye ni miongoni mwa wanaume tajiri zaidi duniani, itachukuliwa na Andy Jassy, ambaye sasa hivi anaongoza biashara ya uhifadhi wa data.


Mabadiliko hayo yatafanyika katika kipindi cha nusu ya pili cha mwaka 2021, taarifa kutoka kampuni hiyo imesema.


"Kuwa Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Amazon ni majukumu muhimu na yenye kuhitaji muda. Ukiwa na jukumu kama hilo. Ni vigumu sana kutoa angalizo kwa mambo mengine," Bwana Bezos amesema katika barua aliyoituma kwa wafanyakazi wa kampuni ya Amazon siku ya Jumanne.


"Kama mwenyekiti nitakuwa najihusisha na mambo mengine muhimu ya kampuni ya Amazon lakini pia nitakuwa na muda na nguvu ya kuangazia miradi ya Day 1 Fund, Bezos Earth Fund, Blue Origin, The Washington Post, na mingine ninayotaka kuikuza zaidi."


"Sikuwa na nguvu inayohitajika lakini hilo halina uhusiano wowote na kustaafu. Nina shauku kubwa juu ya kile ambacho nafikiria kuwa kinaweza kutimizwa na kampuni hii," aliongeza.

 

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger