Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Sababu ya Yanga Kufungiwa na Fifa Hii Hapa

 


IMEELEZWA kuwa Klabu ya Yanga imefungiwa na FIFA kufanya usajili wa misimu mitatu kutokana na madai ya kutomlipa fedha za usajili pamoja na mshahara mchezaji wao wa zamani Amiss Tambwe.

 Kawaida FIFA hutoa adhabu kama hiyo kwa timu zilizoshindwa kutimiza agizo lake na hasa suala la malipo.


Habari za uhakika kabisa kutoka Zurich nchini Uswisi zinaeleza kuwa Yanga ilipewa siku 45 kumlipa mshambuliaji wake wa zamani Amissi Tambwe fedha anazowadai na muda huo ulishapita bila kulipwa.


Yanga bado hawajalipa hata senti kwa Tambwe ambaye anadai dola 19,000 ambazo ni zaidi ya Sh milioni 43.7 na FIFA imewataka Yanga kuongeza asilimia 5 ikiwa kama ya usumbufu kwa mchezaji huyo.


Imeelezwa kuwa Tambwe anadai fedha hizo zikiwa za mishahara ya miezi miwili pamoja na kiasi kidogo ambacho hawakumlipa katika fedha yake ya Usajili.


 

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments