Korea Kusini hawataki utani na Corona, waanza kupima mbwa na paka

advertise hereKorea Kusini hawataki utani na Corona, waanza kupima mbwa na paka
Paka na mbwa katika mji mkuu wa Korea Kusini wataanza kupimwa Covid-19 kama wataonesha dalili, mamlaka ya Seoul imesema.


Golden Retriever dog and British short-haired cats
Hatua hii imekuja wiki chache baada ya taifa hilo kuripoti kisa cha kwanza cha mnyama kuwa na Covid-19 – na mnyama huyo alikuwa paka mdogo.

Ni wanyama wa nyumbani pekee wenye kuonesha dalili kama ya kushidwa kupumua vizuri ndio watapimwa corona.

Wanyama hao lazima watengwe nyumbani kama wakikutwa na maambukizi ya virusi vya corona.

Si lazima kuwapeleka wanyama hao katika eneo la kujitenga kwasababu hakuna ushaidi kuwa maambukizi ya Covid-19 yanaweza kusambaa kutoka kwa binadamu kwenda kwa wanyama, Park Yoo-mi, afisa wa kudhibiti magonjwa alieleza kikao, kwa mujibu wa ripoti ya Yonhap.

Lakini kama mmiliki wa wanyama hao atakuwa amekuwa amelazwa hospitalini kutokana na Covid-19, au wagonjwa sana na hawawezi kuwaangalia , basi wanyama hao watapelekwa katika eneo la kujitenga.

Nchini Korea Kusini , wagonjwa wa Covid-19 huwa wanatengwa katika eneo maalum kama hawahitaji huduma ya hospitali.

Bi Park amewakumbusha wakazi wa eneo hilo kuwatunza wanyama wao kwa kuwaweka mbali na watu wengine kwa mita mbili angalau wakati wanatembea na watu wengine.

Mapema mwezi uliopita, paka aliyekutwa katika kituo cha kanisa katika mji wa kusini mashariki alikuwa ana maambukizi.

Mamlaka ya afya inashuku kuwa mama na binti yake, , ambao walikuwa wanakaa kwenye kituo hicho walimwambukiza paka huyo .

Kwa kuwa wote walikutwa na Covid-19.

Wataalamu walisema awali kuwa si raisi kabisa kwa mbwa au paka kuwaambukiza binadamu virusi, ingawa utafiti unaonesha kuwa paka wanaweza kubeba virusi na kuambukiza paka wengine.

Duniani, paka kadhaa wamepima virusi vya corona – kutokana na kesi za namna hiyo ni nadra kutokea.

Mwezi uliopita, Sokwe wawili huko San Diego katika hifadhi ya Safari walipata Covid-19 kutoka kwa mtu aliyekuwa anawahudumia -hii ilikuwa kesi ya kwanza ya maana ya maambukizi ya sokwe.

Idadi kubwa ya wanyama wengine wa porini wakiwemo simba, chui katika hifadhi ya Bronx mjini New York na simba katika hifadhi ya Barcelona huko Spain.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE