2/06/2021

RC Chalamila: Marufuku kutumia neno kifo cha ghaflaMkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila amesema kumekuwa na tabia iliyojitokeza siku za hivi karibuni kwa wakazi wa Mkoa huo kutoa taarifa katika mitandao ya kijamii ya kifo cha mtu kuwa amekufa ghafla, amesema kuanzia leo hataki kusikia taarifa hizo.

Chalamila ameyasema hayo akiwa Wilayani Kyela katika maadimisho ya Miaka 44 ya kuanzishwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Chalamila amefikia kutoa kauli hiyo baada ya kuona taarifa za namna hiyo zimekuwa zikiongezeka na kupelekea kuleta taharuki katika Mkoa wake, kitu ambacho kitapelekea wageni kutoingia mkoani hapo na kupelekea kukosekana kwa mapato.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

1 comment:

  1. Chalamila, wewe kweli ni kiboko, unaona mbali kama Ole Sabaya na Ali Hapi.
    Kunenge nae anajaribu. Hongera sana. Chapeni Kazi.

    ReplyDelete

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger