Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Unaambiwa Sarah Asepa na Kila Kitu Chake Kwa Harmonize

IMEVUJA! Aliyekuwa mpenzi wa staa wa Bongo Fleva, Rajabu Abdul ‘Harmonize’ Sarah ametimkia nchini kwao Italy na kuchukua kila kilichokuwa chake kwa zilipendwa wake huyo.


Chanzo chetu cha karibu kabisa na mrembo huyo, kimesema kuwa, Sarah aliamua kurudi kwao kwa sababu ya kuchoka na vituko vya Harmo tangu ilipojulikana kuwa ana mtoto wa nje na kuamua kumuweka hadharani.


“Unajua Sarah aliamua kunyoosha mkono juu na kusepa zake nchini kwao maana alishindwa kuvumilia kila kukicha visa hivyo aliona wazi hapendwi wala hathaminiwi,” alisema mtoa habari huyo.Akiendelea kushusha ubuyu kama wote, mtoa habari huyo alisema, Sarah aliamua kuondoka kwa ajili ya kutotaka kukumbuka chochote walichokuwa wakishea na msanii huyo akiwa hapa nchini na kubadilisha mazingira mengine kabisa ili kupunguza machungu aliyokuwa nayo.


“Sarah ameondoka kwao lakini alikuwa na maumivu makali sana akaona bora aondoke labda anaweza kupunguza machungu aliyokuwepo nayo kutokana na Harmonize kumsaliti na kubadilisha kabisa hali ya hewa,” alisema mtu huyo ambaye ni wa karibu na Sarah.


Gazeti hili lilijaribu kumtafuta kwa njia ya meseji ya moja kwa moja kupitia mtandao wake wa Instagram lakini hata hivyo hakutoa ushirikiano wowote.


 DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLESarah na Harmo walioishi kwa miaka kadhaa bila kupata mtoto, walifunga ndoa ya kimila nchini Italy na kufanya tafrija nyingine hapa Bongo kabla ya kumwagana na kila mtu kushika hamsini zake.Kwa sasa Harmo ameonesha kujitosa mzimamzima kwenye penzi la mrembo kutoka Bongo Movies, Kajala Masanja

GPL

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments