Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Watu 32 Wafariki Baada ya Ajali Mbaya za MagariWATU 32 wamepoteza maisha na wengine watano kujeruhiwa vibaya, baada ya ajali mbaya kutokea usiku wa kuamkia leo ikihusisha magari matano likiwemo lililobeba jeneza, katika eneo la Kasese, Magharibi mwa Uganda.

Kwa mujibu wa Msemaji wa Shirika la Msalaba Mwekundu, Irene Nakasita, ajali hiyo imetokea baada ya gari lililokuwa limebeba jeneza liligongana na gari dogo namuda mfupi baadaye, gari jingine lililokuwa limewabeba waombolezaji, lilipoteza mwelekeo na kuyagonga magari yaliyogongana.

Muda mfupi baadaye, malori mawili yaliyokuwa yamebeba saruji, nayo yalipoteza mwelekeo na kuyagonga magari yaliyokuwa yamepata ajali, na kusababisha maafa makubwa.

Majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Kilembe katika wilaya ya Kisese huku baadhi miongoni mwao wakiwa na hali mbaya.
 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments