2/03/2021

Watu 32 wathibitishwa kufariki kwenye ajali ya gari UgandaWatu 32 wamethibitishwa kufariki kwenye ajali ya gari nchini Uganda iliyotokea usiku wa kuamukia leo katika wilaya ya Kasese nchini Uganda.

Vifo hivyo vimetokea baada ya magari matano kugongana katika kijiji cha Kihongo kilichopo kwenye barabara kuu ya Hima –Rugendabara wilayani Kasese magharibi mwa Uganda.

Miili ya marehemu 32 imepatikana na majeruhi watano wamepelekwa katika hospitali ya Kilembe.

Katika taarifa iliyotolewa na shirika la Msalaba mwekundu nchini humo , timu yao ikishirikiana na jeshi la UPDF na Polisi ikiongozwa na Meja Charles Nzei wameweza kuwaokoa majeruhi na kupata miili ya waliofariki.

Sababu ya ajali hiyo imetajwa kuwa ni ufinyu wa barabara inayotengenezwa na kulikuwa giza kubwa na hivyo kusababisha Malori mawili kugongana mjini Kasese na kuanguka.

Baada ya yaliangukakwa malori mawili ambayo tayari , gari lingine kutoka Budibugyo pia likaanguka kwenye katika eneo hilo hilo.

Kwa pamoja magari 5 yakaanguka kwanye ajali iliyosababaisha vifo vya watu 32 na watano kujeruhiwa vibaya majira ya saa tatu za usiku kwa mujibu wa msemaji wa Red Cross Irene Nakasita.

Kati ya magari hayo ,Lori dogo ya aina ya kenta lilikuwa limebeba jeneza na watu waliokuwa wakielekea kwenye mazishi wakitoka wilayani Budibugyo wakielekea Kata ya Maliba.

Kwa mujibu wa takwimu za jeshi la polisi nchini Uganda karibu ajali za barabarani 20,000 hutokea kila mwaka nchini Uganda na kusababisha takribani vifo vya watu 2,000.

Hii inaifanya Uganda kuwa miongoni mwa mataifa yenye kiwango cha juu cha ajali za barabarani. 2/03/2021 03:00:00 PM   Watu 32 wamethibitishwa kufariki kwenye ajali ya gari nchini Uganda iliyotokea usiku wa kuamukia leo katika wilaya ya Kasese nchini Uganda.

Vifo hivyo vimetokea baada ya magari matano kugongana katika kijiji cha Kihongo kilichopo kwenye barabara kuu ya Hima –Rugendabara wilayani Kasese magharibi mwa Uganda.

Miili ya marehemu 32 imepatikana na majeruhi watano wamepelekwa katika hospitali ya Kilembe.

Katika taarifa iliyotolewa na shirika la Msalaba mwekundu nchini humo , timu yao ikishirikiana na jeshi la UPDF na Polisi ikiongozwa na Meja Charles Nzei wameweza kuwaokoa majeruhi na kupata miili ya waliofariki.

Sababu ya ajali hiyo imetajwa kuwa ni ufinyu wa barabara inayotengenezwa na kulikuwa giza kubwa na hivyo kusababisha Malori mawili kugongana mjini Kasese na kuanguka.

Baada ya yaliangukakwa malori mawili ambayo tayari , gari lingine kutoka Budibugyo pia likaanguka kwenye katika eneo hilo hilo.

Kwa pamoja magari 5 yakaanguka kwanye ajali iliyosababaisha vifo vya watu 32 na watano kujeruhiwa vibaya majira ya saa tatu za usiku kwa mujibu wa msemaji wa Red Cross Irene Nakasita.

Kati ya magari hayo ,Lori dogo ya aina ya kenta lilikuwa limebeba jeneza na watu waliokuwa wakielekea kwenye mazishi wakitoka wilayani Budibugyo wakielekea Kata ya Maliba.

Kwa mujibu wa takwimu za jeshi la polisi nchini Uganda karibu ajali za barabarani 20,000 hutokea kila mwaka nchini Uganda na kusababisha takribani vifo vya watu 2,000.

Hii inaifanya Uganda kuwa miongoni mwa mataifa yenye kiwango cha juu cha ajali za barabarani.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger