Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Kigwangalla: Kifo cha Rais Magufuli kimekuja ghafla sana

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mbunge huyo wa Nzega Hamisi Kigwangalla ameandika haya baada ya mazishi ya hayati Rais Magufuli:-Kwenye somo la saikolojia tunafundishwa kushiriki mchakato mzima wa mazishi ili mwisho wa siku tuukubali ukweli kwenye roho zetu. Inasemwa na wataalamu Kama unaweza kulia, basi lia, kama kugalagala, galagala! Hii ni kwa ulinzi wa Afya yako ya akili. Ukijizuia, usishangae kuingia kwenye hatua ya ‘denial’ (kuukataa ukweli), ambayo inaweza kupelekea ukaugua ugonjwa wa akili ujulikanao kama Bipolar Disorder; Depression (ama Sonono). Kifo cha Rais Magufuli kimekuja ghafla sana, kuna wengi tungechelewa kuamini na kukubali kuwa mpendwa wetu ametutoka! Hata hivyo binafsi nashukuru na naipongeza sana serikali Kwa kutupa fursa pana ya kushiriki mchakato wa mazishi kikamilifu. Wengine tumefarijika kushiriki mpaka maziko ya mzee wetu.

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments