Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Mabeyo aliachiwa dokezo na Magufuli kabla ya kifo

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

 


Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo, amemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan, kukutana naye ofisini kwake ili aweze kumuambia dokezo alilodokezwa na aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Magufuli.


Jenerali Mabeyo ametoa kauli hiyo hii leo Machi 26, 2021, Chato mkoani Geita, wakati wa ibada maalum ya mazishi ya Hayati Dkt. John Magufuli, ambaye atazikwa leo alasiri katika makaburi ya familia yaliyopo nyumbani kwake Chato.


"Mheshimiwa Rais (Samia) binafsi Hayati Dkt. Magufuli alinidokeza, lakini ninaomba nisilitoe dokezo hilo hapa nitakuomba nikuone ofisini, " ameeleza Jenerali Venance Mabeyo.


Aidha, Jenerali Mabeyo, amempongeza Rais Samia, na kumuahidi kuwa watahakikisha vyombo vya ulinzi na usalama vinamlinda, "Vyombo vya ulinzi na usalama vinapenda kukuhakikishia kuwa ulinzi wa nchi na mipaka yake ni salama na kwamba vitaendelea kukulinda wewe, kukutii na kutekeleza majukumu yake aidha vinakuhakikishia utiifu, uadilifu na uaminifu mkubwa kwako kama ilivyo mila na desturi ya majeshi yetu". 


TOP STORIES


CURRENT AFFAIRS

Nkurunziza afariki dunia, chanzo chatajwa


CURRENT AFFAIRS

RC Mbeya awatimua Kidato cha 5 na 6 awataka kurudi


ENTERTAINMENT

Seyi Shay ataja orodha ya wanaume alio-date nao


CURRENT AFFAIRS

Kama alivyosema Makonda ''Wameoga'' - Kamwelwe
MOST POPULAR


CURRENT AFFAIRS

Hii ndiyo sababu ya Mama Janeth kutofika Zanzibar


CURRENT AFFAIRS

Samia aeleza maneno aliyoambiwa na Magufuli


CURRENT AFFAIRS

Kauli ya Zitto kabla ya Magufuli kuzikwa


CURRENT AFFAIRS

Hii ndiyo idadi ya waliotazama kuagwa kwa Magufuli


CURRENT AFFAIRS

Mbowe atoa wito huu kwa Watanzania 

ABOUT US

ABOUT USADVERTISEJOBSTERMS & CONDITIONSCONTACT USFREQUENTLY ASKED QUESTIONS

NETWORK

IPP MEDIAEAST AFRICA RADIOITVRADIO ONECAPITAL RADIOLOKOPROMO

© 2021 East Africa Television Limited. All Rights Reserved


Post a Comment

0 Comments