Makonda anajambo la kumuambia Ma

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


 Aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, leo ameandika kauli yake ya kwanza mtandaoni tangu kutokea kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Magufuli, na kusema kuwa atakapoamka kuna jambo atamuambia.

 Kauli hiyo ameandika hii leo Machi 25, 2021, kupitia ukurasa wake wa Instagram, ikiwa zimepita saa kadhaa tu tangu ashiriki kuuaga mwili wa Hayati Dkt. John Magufuli, mkoani Mwanza hapo jana.

"Pamoja na kukuona jana bado moyo wangu unaamini umelala hujafa, rafiki, kaka na kiongozi wangu utakapoamka usingizi kuna jambo nitakwambia," ameandika Makonda.

Hayati Dkt. John Magufuli, alifariki dunia Machi 17, 2021, katika hospitali ya Mzena Dar es Salaam kwa maradhi ya moyo na atazikwa kesho Machi 26 kijijini kwao Chato.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad