Uwanja Wa Ndege Kia Kuwa Lango La Watalii

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA






Wizara ya maliasili na utalii imesema inampango wa kuufanya uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro KIA kuwa lango la kuingilia watalii kutoka nchini mbalimbali wanakuja kujionea vivutio na upekee wa Tanzania. 


Wizara imeweka mikakati wa kuongeza watalii kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo  wa sekta ya usafirishaji ili kufia adhima ya serikali ya awamu ya tano ya kufikisha watalii milioni tano kwa mwaka ifikapo 2025.



Hayo yamesemwa na waziri wa maliasili na utalii Dkt. Damas Ndumbaro katika mkutano na wadau wa utalii katika sekta ya usafirishaji ambapo ameitaja sekta usafirishaji kuwa mhimili mkubwa wa  kuongeza idadi ya watalii nchini. 



Waziri ndumbaro amesema ili watalii kutoka nchi mbalimbali waweze kufika katika hifadhi zetu ni lazima watumie usafiri wa  ndege ama meli,hivyo watawasiliana na wizara ya uchukuzi ili kuona namna ya kuweza kupunguza kodi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa  Kilimanjaro KIA.



Kwa upande wake kaimu  Kamishna wa uhifadhi wa mamlaka ya usimamizi wa Wanyamapori  Tanzania ( TAWA) Mabula Misungwi, amesema wao kama TAWA wamepokea ushauri wa wadau wa utalii na kuahidi kuyafanyia kazi mapendekezo ya wadau ili kukuza sekta  ya utalii wa uwindaji.



Amesema Tanzania inaongoza kwa rasilimali na vivutio vingi ambavyo vingine havipatikani katika maeneo mengine yeyoyote duniani huku akiwataka watalii  kutembelea hifadhi za taifa.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad