Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Baadhi ya Mali za Hotel ya Ngurdoto Zauzwa Kulipia Madeni ya Mishahara Milion 129

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

 


Baadhi ya mali za Hotel ya Kitalii ya Ngurdoto Mountain iliyopo Usa River, Wilayani Arumeru zimetakiwa kupigwa mnada ili kufidia mishahara ya watu 93 waliokuwa Wafanyakazi wa Hoteli ambao wanadai Tsh. Milioni 129


Amri hiyo imetolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Masijala Ndogo ya Kazi. Naibu Msajili wa Mahakama, John Nkwabi alitoa maamuzi hayo Aprili 26 ambapo kesi hiyo yenye namba 140 ya mwaka 2020, ilisajiliwa Oktoba 16 Mwaka 2020


Mali zitakazopigwa mnada ni vitanda 139, Gari aina ya Coaster yenye namba za usajili T847 DPH, kiwanja namba 418 kilichopo Block A eneo la Leganga, Usa River, na mashine nne za kufulia nguo


Dalali wa Mahakama ametakiwa kuzikamata mali hizo na kusuburi amri ya Mahakama itakayotolewa Mei 4, 2021

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments