Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Ndani ya siku 18 za Mama Samia Taifa limejawa na FURAHA ingawa hajagawa pesa barabarani wala kuongeza mshahara ila maneno tu ya faraja

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

 


Ndani ya siku 18 za Urais wa Samia Suluhu, nchi imejawa na FURAHA, siyo kwamba amepandisha mishahara HAPANA, siyo kwamba ameajiri HAPANA, siyo kwamba anagawa pesa huko mitaani HAPANA

bali ni MATAMSHI yake tu kama Kiongozi Mkuu wa nchi yanaendelea kuliponya taifa bila sindano wala vidonge.


Kwenye utawala uliopita taifa liligawanyika vipande vipande, taifa liliumizwa na hata yeye alijua ndiyo maana ameanza kwa kuliponya taifa kwa maneno yake kabla ya vitendo.


Nadhani mama huyu hahitaji kuomba aombewe bali sisi kama taifa kwa imani zetu bila kujali kipato, nafasi/cheo, kanda, kabila ama jinsia tuanze kumwombea afya njema, hekima, busara na nidhamu asiingiwe na kiburi huko mbeleni.


Mafisadi pia mkae mbali na mama, Wanasiasa vigeugeu mkae mbali na mama huyu, Viongozi wa dini vigeugeu mkae mbali na mama huyu, Watendaji wa serikali vigeugeu mkae mbali na mama huyu, Wajinga wajinga mkae mbali na mama huyu, Waandishi wa habari vigeugeu mkae mbali na mama huyu, Matapeli wala rushwa mkae mbali na mama huyu


Hatufurahi kupitiliza ila angalau ukikutana watanzia watano, watatu kama sio wanne wanalotabasamu utasikia mama ....oohh mama ni mtu na nusu .


Mungu Mbariki Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan

Mungu atubariki Watanzania

Mungu Ibariki Tanzania.

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments