Nisha ampongeza Ex wake kwa kufunga ndoa

 Muigizaji wa filamu nchini Salma Jabu 'Nisha' bebee amempongeza Ex wake kwa kufunga ndoa na kusema alikuwa mkweli sana kwake. Nisha pia amewataka wanaume wa Kitanzania wajifunze kutoka kwa Ex wake huyo na waache Uongo.
Ameandika 

"Huyu ni Ex wangu na leo anafunga ndoa na nguo ya harusi ya mkewe mimi ndo nimemuordea, I'm so happy for him.

Kwanini nimeshare hapa? kwanza kama inspiration kwangu na ushuhuda wa mapenzi ya kweli, now yeye ni kama kaka angu na tuko sawa kabisa.

Huyu mwanaume amekuwa mkweli sana na hata kutengana sababu moja wapo (zipo muhimu zngn) tulitengana sababu tu ya utaifa na sikuweza kuacha maisha yangu Tanzania na kwenda nchi ingine kuwa mtu mwengine na hata yeye hivyo hivyo.

Pamoja na yote amekuwa akinambia kila kitu hadi hili kukamilika hadi nguo kuorder na mengineyo.

Nimelileta hili kwenu WANAUME WA KITANZANIA mjifunze, kama Mwanamke unaona huyu si mke wangu kuna kikwazo hiki na kile mchane live na sio kumdanganya, mna msemo wenu Mwanamke bila kudanganywa haendi, acheni hizo fikra potofu, wanawake wote tunaojitambua tunapenda wanaume wakweli, niambie ukweli hata kama utauma vipi, nikipoa ninrahisi kukusamehe kuliko ukinidanganya.

Naomba niwasemee wasanii wa kike wa Tanzania wanaodate na waliowazidi umri au kipato. Wengi wamekuwa wahanga wa kutendwa na walio sawa nao na ndio maana wanaona bora niwe na mtu nnayeweza kumcontrol hata nikiachana Naye siumii kivile sababu ntapata tu kama yeye.

I call it desperate, i was there na nikaona ni ujinga..

Ila UONGO WENU WANAUME NDO UNASABABISHA WANAWAKE WENGI WANAKUWA DESPERATE.. tunawapenda WANAUME ZETU WA KITANZANIA ila PUNGUZENI UONGO NA UHUNI." - Unasomeka ujumbe wa @nishabebee kupitia ukurasa wake wa Instagram.đŸ’¥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SERIKALINI

đŸ’¥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SEKTA BINAFSI

đŸ’¥NAFASI ZA INTERSHIP MAKAMPUNI MBALI MBALI

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad