Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Ulimwengu akimbiza Ligi Kuu Congo DR

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

Mtanzania Thomas Ulimwengu baada ya kukosekana katika michezo kadhaa ya TP Mazembe akisumbuliwa na enka jana amerudi uwanjani na kuisaidia timu yake kupata ushindi wa magoli 4-1 dhidi AC Rangers katika mchezo wa Ligi Kuu Congo DR.
Ulimwengu aliyeibuka Man Of The Match katika mchezo huo alifanikiwa kufunga magoli mawili na kusababisha penati, Ulimwengu amekuwa na changamoto ya kukumbwa na majeruhi mara kadhaa.

Ushindi huo sasa unaifanya TP Mazembe waongoze Ligi kwa kuendelea kuwa vinara kwa point 46, wakiwa wamecheza michezo 20 hadi sasa wakifuatiwa na Maniena wenye point sawa na wao 46, AS Vita akiwa nafasi ya tatu kwa kuwa na point 42 alizovuna katika michezo 18.

Post a Comment

0 Comments