.

5/29/2021

Albam ya DMX yakamilika siku 48 baada ya kifo chakeHatimaye albam ya Nyota wa rap, DMX aliyekuwa amepania kurejea kwa nguvu katika muziki kabla ya kifo chake kilichostua, iko tayari kwa ajili ya kuachiwa leo Ijumaa Mei 28, 2021.


Rapa huyo aliyefariki akiwa na miaka 50 alitamba katika miaka ya tisini na mwanzoni mwa milenia hii akiwa na albamu tano zilizoshika nafasi ya juu katika chati za nyimbo baada ya kuzinduliwa.


Kuna hisia za ukombozi katika albamu hiyo yenye nyimbo 13, mada ambayo inagusa hisia baada ya kifo cha msanii huyo.


DMX hajaweza kuona albamu yake mpya ya “EXODUS” ikiingia sokoni ikiwa imetayarishwa na Def Jam Recordings baada ya kufariki Aprili 9 akiwa hospitalini ambako aliwekewa mashine ya kumsaidia kuendelea kuishi kwa karibu wiki moja kufuatia kupata shambulio la moyo.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger