Mbunge Kishimba: Degree Isomwe Kwa MIEZI Minane tu, Vyuo Vitafutie Wahitimu Ajira

 


Mbunge wa Kahama Mjini, Jumanne Kishimba ameshauri Vyuo Vikuu viwajibike kutafuta ajira kabla ya kusajili Wanafunzi kwasababu Wazazi wengi wamechoshwa na mfumo wa #Elimu unavyofilisi mali zao tofauti na matarajio


Amesema "Leo hii tunaongeza Umasikini baadala ya kuongeza Elimu. Wananchi hawataki tena kusikia mambo ya Shule, Vijijini ukifika ukiuliza Ng'ombe wa hapa wameenda wapi, utaambiwa wamemalizwa na Shule"


Ameongeza "Makampuni yote Duniani yanafanya Biashara na Vyuo Vikuu, hapa Tanzania sijaona Chuo kinachotembelea waajiri. Inawezakana hata ile Elimu wanayotoa Vyuoni si ile inayohitajika kwa waajiri. Tufike mahala badala ya kusoma Degree kwa miaka mitatu wasome kwa miezi nane inatosha"

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE