Morrison Aachwa Safari ya Sauzi

advertise here


NYOTA wanne wa Simba wamebaki Bongo wakati timu hiyo ikikwea pipa kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika unaotarajiwa kuchezwa Mei 15 dhidi ya Kaizer Chiefs.

Kikosi hicho kiliondoka leo alfajiri kuwafuata wapinzani hao kwenye mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Mabingwa Afrika ambapo watapitia Kenya kisha wataunganisha safari yao kuelekea nchini Afrika Kusini.

Kwa mujibu wa Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu ni Perfect Chikwende, Said Ndemla na Miraj Athuman.

“Mwingine ni Morrison ambaye anamalizia taratibu zake, Inshallah Mungu akisaidia atajiunga na sisi kesho. Tunaenda na wachezaji 24, Morrison akijiunga na sisi atakuwa wa 25.”

Usajili wa Chikwende ambaye ni kiungo mshambuliajii aliyekuwa akicheza ndani ya Klabu ya FC Platinum ni maalumu kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu Bara.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE