Urusi yalenga kuharamisha mitandao ya Navalny

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA





Mahakama ya Urusi inajiandaa leo kusikiliza kesi ya kile kinachotajwa kuwa 'misimamo mikali' kwa mtandao wa kisiasa wa mkosoaji wa serikali ya nchi hiyo, Alexei Navalny, ambaye kwa sasa ni mfungwa, mnamo wakati Moscow ikijaribu kuharamisha upinzani dhidi ya Rais Vladimir Putin.
Kesi hiyo itakayosikilizwa faraghani ni sehemu ya operesheni ya Rais Putin dhidi ya mkosoaji wake mkubwa Navalny pamoja na wafuasi wake, na inajiri baada ya jaribio la awali la kuwekewa sumu mwaka uliopita. 

Mwezi uliopita, waendesha mashtaka waliomba mtandao wa Navalny kwenye majimbo pamoja na Wakfu wake wa kupambana na ufisadi, kuorodheshwa kama mashirika yenye misimamo mikali, wakiyatuhumu kupanga maandamano makubwa yanayoungwa mkono na nchi za Magharibi. 

Kama sehemu ya jitihada hizo, baraza la bunge linatarajiwa kuanza kujadili muswada unaopiga marufuku wanachama wa mashirika yanayotajwa kuwa yenye misimamo mikali, kuchaguliwa kama wabunge.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad