Kesi ya ufisadi dhidi ya Jacob Zuma yasogezwa mbele

Kesi ya ufisadi ya Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma imesogezwa hadi 26 Mei ambapo ombi rasmi litawasilishwa.Anatarajiwa kukana mashtaka yanayomkabili.
Wafuasi wa Bw Zuma walikusanyika nje ya Mahakama Kuu ya Pietermaritzburg kabla yeye kujitokeza.

Rais huyo wa zamani anakabiliwa na makosa 16 ya ufisadi unaohusiana na makubaliano ya silaha ya mabilioni ya dola.Jumla ya mashahidi 217 wanatarajiwa kutoa ushahidi dhidi yake.

Kesi hiyo inahusu makubaliano ya biashara ya silaha na kampuni ya silaha ya Ufaransa Thales ambayo ilikuwa na nia ya kuboresha ulinzi wa Afrika Kusini mwishoni mwa miaka ya 1990.

Bw Zuma na kampuni hiyo wamekana mashtaka ambayo ni pamoja na udanganyifu, ulaghai na uhujumu uchumi.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE