Almasi inayoaminika huenda ni ya tatu kwa ukubwa duniani yapatikana Botswana

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA





Almasi inayoaminika kuwa ya tatu kwa ukubwa kuwahi kupatikana imewekwa kwenye maonesho nchini Botswana.
Jiwe hilo la thamani - lenye uzito wa karati 1,098 - lilioneshwa Rais Mokgweetsi Masisi, wiki mbili baada ya kampuni ya Almasi, Debswana, kuipata.

Jiwe hilo ni zito kidogo kuliko almasi ya pili ya ukubwa duniani ambayo pia ilipatikana Botswana mwaka 2015.

Botswana ndio mzalishaji mkubwa wa madini ya almasi Afrika.

"Hili ndio jiwe kubwa la almasi kupatikana na kampuni ya Debswana katika historia yake tangu ilipoanza kuendesha shughuli zaidi ya miaka 50," amesema Lynette Armstrong, kaimu mkurugenzi wa kampuni ya Almasi ya Debswana.

"Kutokana na utafiti wetu wa awali huenda jiwe hilo ndio la tatu kwa ubora duniani."

Debswana ni mshirika wa pamoja kati ya serikali na kampunni kubwa ya madini ya almasi duniani De Beers na hadi asilimia 80 ya kipato kinachotokana na mauzo hayo huelekezwa kwa hazina ya serikali kupitia pesa zinazolipwa kama faida, mrabaha na kodi.

Waziri wa madini nchini Botswana, Lefoko Moagi, amesema ugunduzi huo wa hivi karibuni umewadia wakati muafaka baada ya janga la virusi vya corona lililokumba Botswana kusababisha kupungua kwa mauzo ya almasi mwaka jana.

Jiwe hilo la Almasi kubwa kuwahi kupatikana lilikuwa karati 3,106 aina ya Cullinan huko Afrika Kusini mwaka 1905 na la pili kwa ukubwa ni karati 1,109 la Lesedi La Rona lililopatikana Botswana mwaka 2015.

Jiwe hilo jipya kabisa kupatikana katika mgodi wa Jwaneng bado halijapewa jina.

Bwana Armstrong alisema bado uamuzi haujachukuliwa wa iwapo "jiwe hilo la madini lisilo la kawaida liuzwe" kupitia kampuni ya De Beers au kampuni ya Almasi inayomilikiwa na serikali ya Okavango.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad