.

6/07/2021

Mwanamfalme Harry na mke wake Megan wapata mtoto wa pili
Mwanamfalme Harry Mtawala wa Sussex na mke wake Mergan wametangaza kuzaliwa kwa mtoto wao wa pili, msichana. Lilibet “Lili” Diana Mountbatten-Windsor alizaliwa Ijumaa asubuhi katika hospitali ya Santa Barbara, California.Mama na mtoto wake katika hali nzuri ya kiafya, ilisema taarifa ya wanandoa hao.

Kasri ya Buckingham Palace imesema: “Malkia, Manamfalme wa Wales na Duchess wa Cornwall, na mtawala wa Cambridge na mkewe wamefahamishwa na wamefurahishwa na taarifa hizo.”Mwanamfalme Harry na Meghan wamesema wamempatia mtoto wao wa pili jina la Lilibet ambalo ni jina la utani la Familia ya Kifalme kwa Malkia.

Jina lake la kati, Diana, lilichaguliwa kumuenzi “bibi yake mpendwa”, Malkia wa Wales.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger