Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Wanafunzi watekwa nyara Nigeria
Takribani wanafunzi 150, hawajulikani walipo baada ya watu waliokuwa na silaha kuvamia shule ya bweni katika jimbo la kaduna nchini Nigeria na kutokomea nao kusikojulikana.Jeshi la Polisi kwa kushirikiana  na wanajeshi wanawasaka wanafunzi hao. Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, shule hiyo ya upili ya Bethel Baptist ni ya 10 kushambuliwa kaskazini magharibi mwa Nigeria tangu Desemba, wakati mamlaka zikisema kuwa washambuliaji hudai fidia baada ya kuwateka nyara wanafunzi.

Ripoti zinasema kuwa idadi kubwa ya wazazi waliokuwa wakilia walikusanyika kwenye shule hiyo, wakitarajia kupata taarifa kuhusiana na waliko watoto wao. Ripoti za polisi zinasema kuwa washambuliaji waliingia saa za usiku na kuwazidi nguvu walinzi waliokuwepo huku wakitoroka na wanafunzi kuelekea kwenye msitu ulio karibu.

Hata hivyo taarifa zimeongeza kusema kuwa watu 26 akiwemo mwalimu mmoja wa kike wameokolewa. Mwanazilishi wa shule hiyo kasisi John Hayab ameiambia Reuters kwamba takriban watu 25 walibahatika kuponyoka wakati wanafunzi waliobaki walishikwa mateka na washambuliaji.

BY BAKARI WAZIRI

 HABARI KAMA HIZI DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL KWA KUBONYEZA > HAPA

Post a Comment

0 Comments