Milango yetu ipo wazi kukutana na Rais - CHADEMA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema milango yake ya kukutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, bado ipo wazi na kuwa wanachosubiri ni ofisi ya Ikulu kuwajibu juu ya tarehe ya Rais kukutana na chama hicho.

Akizungumza na vyombo vya habari Katibu Mkuu wa CHADEMA Bw. John Mnyika amesema kuna mambo mengi yaliyojitokeza ukiachilia mbali masuala ya uchaguzi 2020 ambayo yanahitaji mazungumzo.

"Ni muhimu tukaeeleza wazi milango yetu sisi CHADEMA kukutana na rais bado ipo wazi tunachosubiri ni Ikulu kuweza kututaarifu kama Rais yupo tayari kukutana vyama vya siasa kama alivyoahidi na Chadema tupo tayari,” amesema Bw. Mnyika.

Bw. Mnyika ameongeza kuwa “Kuna mambo yaliyojitokeza na uchaguzi 2020 sasa yamejitokeza mambo mengine zaidi yenye uharaka wa mazungumzo sisi kama Chadema hatujafunga milango ya makutano na rais". 

Akijibu swali aliloulizwa na waandishi kuhusu Katiba mpa, Mnyika amesema suala la Katiba ni kilo cha wananchi na sio cha CHADEMA.

"Katiba mpya imekuwa kilio cha wananchi kwa muda mrefu kuna ushahidi wa moja kwa moja wakati wa mchakato wa Katiba tume ya mabadiliko ya Katiba chini ya Jaji Warioba ilivyozunguka na kukusanya maoni ya wananchi, wananchi walisema wanataka Katiba mpya na Katiba ya iana gani?" amesema Bw. Mnyika.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad