.

8/10/2021

Miquissone Kubaki Simba? Al Ahly Yampotezea

JARIBIO la Mabingwa wa Klabu Bingwa Barani Afrika, Al Ahly ya Misri πŸ‡ͺπŸ‡¬ kupata saini ya Luis Miquissone wa Simba Sc πŸ‡²πŸ‡Ώ huenda likagonga mwamba licha ya kutoa Ofa kwa Klabu ya Simba SC πŸ‡ΉπŸ‡Ώ ya zaidi ya bilioni 2 (dola za Marekani 900,000).

Mabingwa hao wa Kihistoria Barani Afrika kwa sasa wamekaa kimya kuhusu dili hilo huku ikielezwa kuwa nguvu yao kubwa sasa wameielekeza kupata saini ya winga wa Kimataifa wa Afrika Kusini, Percy Tau πŸ‡ΏπŸ‡¦.

 

Kocha wa Ahly Pitso Mosimane alitaka kunasa saini ya Miquissone ambaye ni raia wa Msumbiji kwa miaka minne baada ya Konde Boy huyo kuonyesha kiwango cha hali ya juu katika michuano ya Mabingwa Afrika ambapo Miquissone aliifunga Ahly bao pekee walipokutana na Simba katika Dimba la Mkapa kwenye hatua ya makundi.

 

Taarifa kuhusu uhamisho wa Tau kutoka Brighton and Hove Albion ya Ligi Kuu ya Uingereza kwenda Al Ahly imeshika kasi nchini humo ambapo inaelezwa kuwa Mosimane amependa uchezaji wa Tau anayemfananisha na Lionel Messi.

 

Akizungumza na Goal.Com, Mosimane amesema; “Percy yupo imara kama Messi, ana vitu vingi vya kukupa kila wiki, acha tumpe nafasi,” amesema Mosimane.

 

Kwa upande wake, kuhusu Luis Miquissone πŸ‡²πŸ‡Ώ kujiunga na Klabu ya Al Ahly πŸ‡ͺπŸ‡¬ Klabu ya Simba SC 🦁 imesema itatangaza hivi Karibuni kama amejiunga na Al Ahly πŸ‡ͺπŸ‡¬ au anabaki Simba SC.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger