.

8/24/2021

Mwanamke mmoja amshutumu R.Kelly kuwa alimlazimisha kutoa mimba
Mlalamikaji wa pili alisimama katika kesi ya unyanyasaji wa kijinsia ya R. Kelly Jumatatu, akishuhudia kwamba nyota huyo alimnyanyasa, akimwambukiza malengelenge na akamwamuru atoe mimba.

Mwanamke huyo, aliyejulikana kama Jane Doe No 5, alisema uhusiano wake wa miaka mitano na Bwana Kelly ulianza mnamo mwaka 2014, akiwa na miaka 17.

Alidai kuwa mwimbaji huyo alikuwa akitafuta kuyadhibiti maisha yake na alikuwa akimuadhibu alipokuwa hatii.

Bw.Kelly mwenye miaka 54 amekana shutuma dhidi yake.

Mawakili wake wamewaelezea washtaki kama vikundi vya kulipiza kisasi baada ya uhusiano wao na mwimbaji wa R&B kufa.

 

OPEN IN BROWSER
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger