Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Akutwa Amenyongwa Na Kufungwa Na Kufuli Juu Ya Mti
Mtu mmoja ambaye jina lake halijafahamika kwa haraka amekutwa amening’inizwa juu ya mti mtaa wa Malingumu Mjini Mafinga huku taarifa za kifo chake zikiwa bado hazijajulikana .

 

Kijana huyo anayekadriwa kuwa na umri wa kuanzia miaka 22 ambaye kwa jina la utani anafahamika kama Babu Rungu amekutwa na umauti katika mazingira ya kutatanisha kama anavyobainisha Bi Beatrice Msigwa ambaye alikuwa mtu wa kwanza kufika kwenye tukio.

 

Mwenyekiti wa Mtaa wa Malingumu Frida Kipangula anasema tukio hilo ni tukio la kinyama ambalo halikubaliki hivyo watekelezaji wa tukio hilo lazima watatiwa mbaroni na hakuna ataye salia salama.

 

Hata hivyo baada ya  taarifa za tukio hili kulifikia jeshi la polisi, maofisa wa jeshi hilo waliwasili,ili haraka eneo la tukio na kuondoka na mwili wa marehemu kwa taratibu zaidi za kiuchunguzi ili kubaini chanzo cha tukio hilo na washtakiwa wa utekelezaji wa tukio kuanza kusakwa. Mara moja

 HABARI KAMA HIZI DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL KWA KUBONYEZA > HAPA

Post a Comment

0 Comments