.

9/04/2021

Kajala Agonga Mwamba, Aliyepost Picha ya Paula Kwenye Cover Wimbo Agoma Kuifuta..Baada ya msanii wa Bongo Flava aliyegeukia upande wa Singeli, @shebbylove1tz kutumia picha ambayo kwa madai ya @kajalafrida ni picha ya mwanae, Paula kama kava ya wimbo wake mpya unaoitwa KITU,Kajala alimjia juu na kutaka afute Picha hiyo mara moja kabla mambo hayajawa mabaya akimtumia voice note upande wa DM huku akimpa masaa 24 pekee.

Hadi sasa ni Siku ya pili,Shebby hajafuta picha hiyo na wakati anahojiwa amedai yeye kaipata kwenye social networks kama picha nyingine tu na hawezi futa,akitaka alete uthibitisho kama huyo ni mwanae na hata kama ni mwanae basi kutumia picha yake maana yake ni kuwa Shebby ni shabiki wa Paula.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger