Kimeumana... Ndugai atishia kuifumua kamati ya Bunge ya Bajeti

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPADodoma. Spika wa Bunge, Job Ndugai ametishia kuifumua Kamati ya Bunge ya Bajeti baada ya kukerwa na kupitishwa kwa sheria inayoruhusu Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) kuanza kutoza ushuru wa bidhaa wa asilimia mbili kwa mazao nchini.

Spika Ndugai ameyasema hayo leo Jumatatu Septemba 6, 2021 bungeni mara baada ya majibu ya Wizara ya Kilimo yaliyotokana na swali la nyongeza la Mbunge wa Namtumbo (CCM), Vita Kawawa.

Kawawa amesema wakulima wa tumbaku wamekuwa wanalipa ushuru wa wilaya wa mazao, tozo ya vyama vikuu vya ushirika, chama cha msingi.

Amehoji kama ni kweli kuwa TRA mwaka huu itaanza kuwatoza wakulima wa tumbaku ushuru wa bidhaa.


Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema ni kweli Bunge lilipitisha sheria ya ushuru wa bidhaa wa asilimia mbili kwenye mazao ya kilimo.

Hata hivyo, amesema bado wizara haijaanza kukata ushuru huo kwasababu mjengeko wa bei ya tumbaku huamuliwa kati ya Februari hadi Aprili.
Amesema wakati sheria hiyo inapitishwa tayari mjengeko wa bei wa zao hilo ulikuwa umeshapitishwa.

Hata hivyo, amesema wizara yake imewasiliana na Wizara ya Fedha na Mipango kwa kuwaandikia ili kuona namna gani watatekeleza sheria hiyo lakini kwa kulinda maslahi ya wakulima wa zao hilo.


Ndugai amesema wajumbe wa bajeti wanapaswa kuwa makini sana katika kazi zao kwasababu mambo yakifika bungeni wanaiamini kamati.

“Mkiendelea hivi nitaifumua hiyo, kamati ya bajeti tumeweka watu tunaowaamini sana. Sasa kama mnaenda kule mnalala tu na kupitisha tu vitu vya kienyeji mnatuponza. mnapitishaje kitu kama hiyo bwana,”amesema.
________________

KISASI CHA USALITI PENZINI !!!,usipoipenda simulizi hii dai Mb na pesa zako,licha ya kuenjoy mahaba ndani yake kuna kitu cha kujifunza mwishoni Bofya Hapa kusoma Sehem ya 1 bure,sehem iliyobaki tsh 2000 kwa mtandao wowote.

Tembelea www.makapedia.com kwa stori mpya kila tarehe moja.


JE UNATAKA BIASHARA YAKO IWE YA UHAKIKA MIAKA YOTE YAJUE HAYA? usikose kitabu hiki Bofya Hapa kusoma sehem ya 1 bure sehem ya 2 tsh 2000 tu 

ndani ya www.makapedia.com

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad