Kipa wa Yanga Farouk Shikalo asajiliwa KMCFAROUK Shikalo aliyekuwa kipa namba mbili wa Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi leo Septemba 4 ametambulishwa kuwa mali ya KMC.
Nyota huyo ambaye alikuwa anakipiga Yanga mkataba wake wa miaka miwili ulimeguka na mabosi wa timu hiyo waliamua kumuacha aende.

Hakuwa katika nafasi ya kudumu msimu uliopita kwa kuwa katika mechi 34 alikaa langoni kwenye mechi 10 za Ligi Kuu Bara.

Aliweza kutwaa taji la Mapinduzi katika mchezo wa fainali uliochezwa Visiwani Zanzibar mbele ya Simba.

Anakwenda kuungana na kipa namba moja Tanzania, Juma Kaseja ambaye ni nahodha wa kikosi cha KMC ambacho kimeweka kambi Morogoro.

đŸ’¥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SERIKALINI

đŸ’¥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SEKTA BINAFSI

đŸ’¥NAFASI ZA INTERSHIP MAKAMPUNI MBALI MBALI

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad