Uzinduzi wa Jezi za Simba Wayeyuka Mazima

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA
 


 UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa tukio la sherehe za uzinduzi wa jezi ambao ulitarajiwa kufanyika leo Septemba 4 umeyeyuka.

Awali Simba waliwatangazia mashabiki wao kwamba mpango wao namba moja kwenye shughuli ya kutambulisha uzi mpya itakuwa ni Septemba 4, saa 1:00 usiku.

Jana Septemba 3, Simba kupitia kwa Kaimu Ofisa Habari, Ezekiel Kamwaga waliweza kutoa taarifa ya mshtuko kwamba uzi wa Simba upo kwenye maduka yote ya Vunja Bei.

Pia iliwekwa wazi kwamba leo tukio la uzinduzi wa jezi litaendelea kama kawaida saa 1:00 na utaratibu ungetolewa leo.


 
Muda mchache kabla ya shughuli kufika taarifa imetolewa kwa Simba kughairi uwepo wa tukio hilo.

Taarifa hiyo imeeleza:"Tukio la uzinduzi wa jezi rasmi za Simba kwa msimu wa 2021/22 lililopangwa kufanyika leo limeahirishwa.

"Matukio yote ya sherehe sasa yatafanyika wakati wa Wiki ya Simba inayoanza Septemba 13 hadi 19.".

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA


 JINSI YA KUANDIKA CV BORA BONYEZA HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad