Masau Bwire Avaa Nembo ya Simba

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA


OFISA Habari wa Timu ya Ruvu Shooting, Masau Bwire ambaye anatajwa kuibukia mitaa ya Msimbazi kuwa mrithi wa mikoba ya Haji Manara ambaye kwa sasa anaitumikia Yanga kama Ofisa Habari.

 

Hivi karibuni ziliibuka tetesi kwamba Masau ameshamalizana na Simba na ni suala la muda kwake kutangazwa kuwa mali ya timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes pamoja na Seleman Matola ambaye ni msaidizi sawa na Hitimana Thiery ambaye ametambulishwa hivi karibuni.

 

Kwenye shughuli ya kumuaga Hanspoppe Zacharia, leo ukumbi wa Karimjee, Masau alivaa barakoa yenye nembo ya Simba jambo ambalo limeongeza maswali na pia kuna picha ambayo inasambaa ikimuonyesha akiwa na Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez.

 

Akizungumzia suala hilo Masau amesema:”Nimekuja kwenye shughuli ya Simba na nilikuwa na barakoa yangu ila viongozi wa Simba walinifuata na kunipa barakoa.

 

“Mimi ninanidhamu na kila mmoja huwa ninamheshimu hivyo kwa kuwa wenye shughuli wameandaa utaratibu basi nikaamua kutoa barakoa yangu na kuvaa barakoa ya Simba,”amesema Masau.

 

Simba inatarajia kufanya utambulisho wa wachezaji wake pamoja na uzi mpya kwa msimu wa 2021/22 Septemba 19, Uwanja wa Mkapa. NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA


 JINSI YA KUANDIKA CV BORA BONYEZA HAPA 

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad