Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Unaambiwa Blue Hataki Kusikia Neno Management Kabisa "Walinidhulumu Kisa Usogo Wangu"Hivi ni Lini ulisikia Babylon Byser, @mrbluebyser1988 yupo kwenye Management fulani anasongesha life ya Muziki wake? Je unaijua sababu?.

Mr. Blue ni moja ya wasanii wachache walioanza muziki wakiwa na umri mdogo sana. Kipaji chake kilishawishi watu wenye vinasaba vya usimamiaji wasanii wamvute Byser na kuishi nae. Na wakati huo alitoa hits kibao na zilizompa show za maana East Afrika ila matunda yake yakawa yeye kwenda chini huku Management ikienda juu kama Pierre Liquid. Management ilitake advantage sababu ya Umri wake maana alikuwa anatoa shikamoo kwa boss,producers hadi kwa machawa wao.

Star huyo ambaye starehe yake kubwa ni kudondosha mijengo ilifika hatua Management ilimpoteza kabisa kwenye ramani ya muziki na akurudi kitaa akiwa hana kitu,yani apeche alolo wakati maboss wake wanakula vyuku kwenye mijengo ya nyota 5. Ilimchukua muda kurudi kwenye Game na wimbo wa Pesa ndio likawa tobo lake kwa mara ya pili kwenye huu muziki wenye fitina zisizo isha.

Blue anahit bila promo ya ngoma zake,hana Media tour bali anachokifanya anampa mtu mmoja tu ngoma yake apeleke sehemu husika alafu raia watakutana nayo mbele kwa mbele,Hii ndio aina ya utoaji wa kazi zake ambayo alianza nayo kwenye wimbo wa Pesa huku akimshukuru @bdozen kwa kuipokea ngoma hiyo na kwa mara ya kwanza ikachezwa kwenye radio station na watu wakaishi nayo.

Blue ana mpango wa kuanzisha label ambayo hatomtoza mtu hata Senti, lengo kubwa ni kusaidia na kusogeza vipaji mjini, vipaji ambavyo vipo pale vimepigwa stop light za kwenye mataa.

 HABARI KAMA HIZI DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL KWA KUBONYEZA > HAPA

Post a Comment

0 Comments