Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Zamaradi Mketema Afunguka Wimbi la Wasanii Kujenga Mijengo Kigamboni


Aunty Ezekiel ashusha mjengo wake Kigamboni, Dar. Zamaradi Mketema aliweka post akisema ameipenda Kigamboni kuhusiana na ujenzi na makazi. Kisha baadaye kurudi na post nyingine ambayo miongoni mwa aliyogusia ni baadhi ya watu maarufu waliojenga huko akiwemo Aunty Ezekiel, kina Joti etc

"Huenda ndio sababu Kaka zetu wa Ze Comedy enzi hizo waliwahi kuona hiyo fursa mapema na kujenga huko, walikuwa wajanja sana wale 😄, watu kama kina Joti na Mpoki!!, japo kwasasa wameongezeka, katika watu ninaowajua wengine mtu kama Dahuubamejenga Kigamboni, Aunty Ezekiel amejenga Kigamboni, Kaka Yangu Mrisho Mpoto amejenga Kigamboni

Hao ni wale mashuhuri tu lakini kuna wengi ambao hawako kwenye Circle ya Wasanii na ni watu wazito ambao wamejenga Kigamboni, mwanzo sikuelewa sababu, ila baada ya pitapita nimeelewa sababu" ameandika Zamaradi

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments