Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Balaa! Samaki aua sita Zanzibar, walimvua na kumla kwa siri

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE
JUMLA ya watu sita wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 11 wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya ya Micheweni baada ya kula samaki aina ya kasa anayesadikiwa kuwa na sumu katika kijiji cha Msuka Taponi, Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba. Anaripoti Mwandishi Wetu, Pemba … (endelea)

Akizungumza na Mwanahalisi Online, Kamanda wa Polisi mkoa wa Kaskazini Pemba, Juma Sadi Khamis amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa samaki huyo alivuliwa kwa siri tarehe 24 Novemba mwaka huu.

Amesema kwa mujibu wa utaratibu, samaki huyo haruhusiwi kuvuliwa, lakini wavuvi walimvua kwa siri na kwenda kumtoa sumu wenyewe kwa namna wanavyojua.

“Kwa sababu inadaiwa alivuliwa tarehe 24, wakamchemsha na kumlaza kisha tarehe 25 wakamla, madhara yakaanza kujitokeza tarehe 26 na 27 kwa watu watano kufariki na leo tarehe 28 asubuhi amefariki mzee anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 70.


 
“Huyu samaki ana sumu mbaya ndio haruhusiwi kuliwa, lakini wamevua kwa siri na ukiangalia waliofariki walikuwa na umri wa miaka sita hadi 12 lakini sasa mzee wa miaka 70 amefariki,” alisema.
Amesema awali walifikishwa hospitalini zaidi ya watu 22, lakini baada ya kufariki watu sita, wengine walitibiwa na kutoka hospitalini lakini waliobaki ni 11.

Aidha, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ametoa salamu za rambirambi kwa familia za marehemu watatu waliofariki kufuatia kula samaki huyo aina ya kasa.


Katika salamu hizo za rambirambi alizozitoa leo tarehe 28 Novemba, 2021, Rais Dk. Mwinyi ameeleza kusikitishwa na vifo hivyo na kuzitaka familia za marehemu hao kuwa na subira na ustahamilivu katika kipindi hiki kigumu cha misiba hiyo.

“Naziomba familia za marehemu kuwa na subira katika kipindi hiki kigumu cha msiba. Inna lilahi wa inna ilayhi raji’un” ameandika Dk. Mwinyi katika ukurasa akaunti yake ya twitter

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments