Kijana mweusi aliyefungwa kimakosa kwa kufananishwa na mshukiwa mzungu mzee

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Kijana mweusi wa Nevada nchini Marekani alitumikia kifungo cha miaka sita gerezani baada ya polisi kumfananisha kimakosa na mshukiwa mzungu mwenye jina sawa na lake ambaye ana umri mkubwa mara mbili ya umri wake, mashitaka yameeleza.

Shane Lee Brown, mwenye umri wa miaka 25, alikamatwa mwezi Januari 2020 barabarani baada ya kushindwa kuonyesha kibali cha kuendesha gari (licence). Polisi wa Las Vegas walipata kibali kilichoandikwa kwa jina lake.

Lakini kibali hicho kilikuwa ni kwa jili ya Shane Neal Brown halisi, mwanaume wa makamo mzungu mwenye ndevu, yalidai mashitaka ya kesi iliyofunguliwa kuhusiana na tukio hilo.

Kijana huyo hakushitakiwa kwa uhalifu na sasa amewasilisha kesi ya uharibifu uliosababishwa na kufungwa kwake bila kosa.


 
Msemaji wa mji wa Henderson aliviambia vyombo vya habari vya Marekani kwamba kijana huyo alikamatwa kisheria kwa kuendesha gari huku akiwa na kibali kilichosimamishwa.

Mji Henderson haukuelezea kuhusu madai ya kukosewa kwa utambulisho katika hatua za kisheria zilizochukuliwa.

Kulingana na waraka wa kesi hiyo, maafisa wa polisi walisema walifikiria kimakosa kwamba BwBrown alikuwa ni Shane Neal Brown, mwanaume mzungu mwenye nywele za rangi ya kahawia, macho ya blu na ndevu.


Akiwa sasa na umri wa miaka 51, alifungwa kwa uhalifu mwaka 1994, kabla hata Brown mdogo hajazaliwa, vimeripoti vyombo vya habari vya Marekani.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad