Jinsi Kumshikia Mtu zamu ya Kuuza Duka Kulivyosababisha BINTI Huyu Akawa Mke wa Cristiano Ronaldo - Part 1

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



GEORGINA UDHURU ILIMPA RONALDO

Kwenye Maduka ya Gucci Jijini Madrid maeneo ya Saletana ndipo ambapo Binti Georgina Rodriguez alikuwa akifanya kazi Gucci Stores kama Sales Assistant

Jioni moja ya 2016 alipokea simu kutoka kwa Mfanyakazi Mwenzie kuwa yeye amesafiri hivyo anaomba abaki dukani Kuna Mteja anakuja kununua Makoti mazito ya baridi, ilibidi Gio amhudumie

Wakati wafanyakazi wengi walioingia asubuhi wameondoka aliesalia yeye huku kigiza kikianza kuingia, ghafla anaona kundi la Wanaume wanaingia dukani kununua bidhaa

Mbele yake anakutana na Cristiano Ronaldo, Supastaa Mkubwa wa dunia akiwa ameambatana na Kaka yake Hugo na Kijana wake Cristianinho pamoja na 'Chawa' kadhaa😃 hakuamini macho yake

Katika hali ya mshangao, Mtoto wa Ronaldo huyu Cristianinho ndie aliewahi kumsogelea kisha akamsalimia kwa lugha ya kishkaji sana😃 alimwambia "Hi" na Binti akaitikia, kwakuwa alikuwa na umbo dogo na Mdogo pia

Cristiano Ronaldo na Kaka yake wakamsalimia pia kisha wakatazamana kidogo kati ya Ronaldo na Gio kisha Wana wakachukua bidhaa wakaondoka zao, ila ikawa Ronaldo anarudi sana pale dukani

Mpaka siku moja wakakutana tena kwenye maonesho ya mavazi hapo hapo Madrid ndipo hapo Ronaldo alimuita kisha kumuuliza kama wanaweza kutoka kwa ajili ya chakula cha jioni

Gio anasema Ronaldo hakutumia ukubwa wa jina lake bali heshima kama Mwanaume yoyote kwenye kumtongoza Mwanamke, anasema Ronaldo hakumtongoza ila matukio yake tu ilitosha Binti kumpa moyo wake

Siku moja jioni wakati mapenzi yao yanaanza kuchipua na hisia kugongana......

ITAENDELEA PART 2

@jr_farhanjr
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad