Simba Wafanya Mauaji ya Kutisha, Mabao 7, Chama Aondoka na Matatu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Clatous Chama amefunga ‘Hat-trick’ ya tisa katika michuano ya kombe la shirikisho (ASFC) baada ya kuingia kambani mara tatu timu yake ikiibuka na ushindi wa bao 7-0.

Simba wameibuka na ushindi huo dhidi ya Ruvu Shooting na kutinga hatua ya robo fainali na kuungana na Azam FC, Coastal Union, Kagera Sugar, Geita Gold,Yanga, Polisi Tanzania na Pamba.

Mabao hayo yanamfanya Chama kuungana na kina Abdul Suleiman ‘Sopu”, Kinda wa Tunduru Korosho wameingia kambani mara nne, Reliants Lusajo wa Namungo, Eliya Chibula Tunduru Korosho, Meshack Abraham Kagera Sugar, Paul Peter Azam FC.

Wengine waliofunga mabao hayo 'Hati-triki' ni Idd Kipagwile wa KMC alipocheka na nyavu mara tatu wakati timu yake ikiiadhibu Majimaji mabao 4-1, huku Boban Zirintunsya naye akitupia matatu, Mtibwa Sugar ilipoilaza Tunduma United mabao 7-1.

Kama haitoshi naye staa wa Yanga, Heritier Makambo hakuwa mbali kuingia kwenye orodha ya wakali wa 'Hati-triki' alipoiongoza timu yake kutupia mabao 4-0 dhidi ya Ihefu huku yeye akiingia wavuni mara tatu na Fiston Mayele akihitimisha karamu ya mabao hayo.

Katika mchezo wa Simba uliopigwa uwanja wa Mkapa, mbali na Chama kuingia kambani mara tatu mabao mengine yalifungwa na John Bocco (2), Jimmyson Mwanuke moja na Michael Masinda ambaye alijifunga.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad