Davido Aweka Wazi "Sina Mpango wa Kuwa Mwanasiasa"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Nyota wa muziki kutoka nchini Nigeria Davido amesema kuwa hana mpango wa kuingia kwenye siasa kwa sababu kufanya hivyo kutafuta yote mazuri na makubwa aliyofanya kwenye tasnia ya burudani.

Mkali huyo ambaye mwishoni mwa wikiendi alikua na show jijini London, Uingereza ndani ya ukumbi wa 02, amesema mbali na muziki anapenda habari na siasa, lakini hana mpango wa kuwa mwanasiasa kwani siasa nchini mwao ni vurugu.

“Siwezi kuharibu miaka yangu yote ya kuburudisha, kuwafanya watu kuwa na furaha, nibadili na kuwa mwanasiasa na yote niliyofanya kama Davido, na kila kizuri nilichojifanyia vipotee, kwani najua hicho ndicho kitakachotokea,” amesema Davido kwenye mahojiano yake na shirika la habari la BBC, Uingereza.

Sanjali na hilo, Davido alieleza kwa ufupi kuhusu namna familia yake ilivyo ambapo amesema, njia alivyoichukua ni tofauti kabisa kwani alitarajiwa asome, na atakapohitimu akamsaidie baba yake, ambaye ni mfanyabiashara, kwenye kazi zake.

Ameeleza zaidi kwamba awali baba yake alikuwa na mashaka na uchaguzi wake, lakini hofu yake iliisha alipoachia wimbo wake wa Dami Duro mwaka 2012, ambao ulimtambulisha kwenye muziki.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad