3/04/2022

Kauli ya Kwanza ya Freeman Mbowe Akitoka Gerezani

Nafasi za Ajira Jiunge Group la Telegram la AJIRA YAKO Kwa Kubonyeza >> HAPA
Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amewaambia waandishi wa habari waliomfuata kutoka gerezani hadi nyumbani kwake kuwa sasa ni wakati wa kunyamaza, lakini atakuja kuzungumza na viongozi na baadaye vyombo vya habari.

Mbowe aliyekuwa akinukuu maandiko ya Biblia, amewashukuru watu waliomwombea tangu alipokamatwa Julai 2021 na hatimate kesi yake imefutwa leo Machi 4, 2022.


“Kitabu cha biblia cha Mhubiri mlango wa tatu kinasema, kila jambo lina wakati wake chini ya mbingu; kuna wakati wa kusema na kuna wakati wa kunyamaza. Leo niruhusini ninyamaze lakini nitazungumza na viongozi wangu wa chama tutapanga wakati mzuri wa kuznugumza na waandishi wa habari asanteni kwa sala zenu,” amesema Mbowe.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger