Ticker

6/recent/ticker-posts

Mtoto Amkatakata Baba yake Kwa Shoka

 Habari Kama Hizi Zinapatikana UDAKU SPECIAL App, Download HAPA Bure: Link here>>>Jeshi la Polisi mkoa wa Tabora linamshikilia kijana Michael Jacobo (25) mkazi wa Kijiji cha Upungu wilaya ya Nzega kwa tuhuma kumuua baba yake mzazi Jacobo Lubela, baada ya kumvizia majira ya jioni akiwa nje ya nyumba na kumkata shoka kichwani, shingoni na mikono yote miwili.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Richard Abwao, amesema tukio hilo limetokana na imani za kishirikina ambapo mtuhumiwa amekuwa akisumbuliwa na tatizo la ugonjwa wa kifafa ambao amekuwa akiuhusisha kulogwa na baba yake mzazi .

Kamanda Abwao amesema mtuhumiwa huyo baada ya kutiwa nguvuni alihojiwa na kukili kutekeleza mauaji hayo ambapo kwa sasa zinafanyika taratibu za kumfikisha mahakamani.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

________________________________

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments