3/20/2022

Mungu Tunusuri na Hizi Ajali...Ajali Nyingine ya Wawili MorogoroGari aina ya Coaster lililokuwa limebeba abiria likitokea Dar Es Salaamu kuelekea Jijini Dodoma likiwa linaondolewa barabarani baada ya kupata ajali barabara kuu ya Morogoro - Dar es Salaam. Picha Lilian Lucas

Morogoro. Zikiwa zimepita siku mbili tangu ajali ya basi na lori na kusababisha vifo vya watu 23 mkoani Morogoro, ajali nyingine ya gari ndogo ya abiria aina ya Coaster imetokea na kusababisha vifo vya watu wawili katika eneo la Oilcom Nanenane mkoani Morogoro.

Ajali hiyo imetokea leo Jumapili Machi 20, 2022 alfajiri huku chanzo cha ajali hiyo kikidaiwa kuwa ni mwendo kasi wa dereva wa Coaster ambaye amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro.

Majeruhi wa ajali hiyo, Msafiri Msafiri akizungumza na Mwananchi amesema tangu wameanza safari Mbezi jijini Dar es Salaamu dereva alikuwa mwendo kasi pamoja kumtaka asiendeshe hivyo mara kwa mara.

Muuguzi kiongozi wa zamu hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro, Joyce Kiwale amesema walipokea majeruhi 17 ambapo kati yao watu wawili wanaume wamefariki dunia wakati wakipata matibabu hospitalini hapo.

Amesema hali za majeruhi wengine zinaendelea vizuri kwani kuna waliopata majeraha madogo kwenye miili yao yakiwamo ya michubuko.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Fortunatus Muslimu amethibitisha kitokea kwa ajali hiyo na kwamba taarifa kamili ataitoa baadaye.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger