Samia awaondoa hofu Chato

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



RAIS Samia Suluhu Hassan amewatoa hofu wananchi wa Chato kwamba miradi yote iliyopangwa  na iliyoanza  kutekelezwa wilayani hapo itakamilika kama ilivyopangwa.

Miradi hiyo ni ile iliyoanzishwa na serikali ya awamu ya tano chini ya Hayati Rais John Magufuli kama vile uwanja wa ndege, stendi ya mabasi hospitali ya rufani ya kanda na uwanja wa michezo.

Samia aliyasema hayo jana mjini hapo wakati wa kumbukizi ya mwaka mmoja wa kifo cha Hayati Magufuli iliyofanyika uwanja wa michezo Chato iliyoambatana na ibada maalum iliyoongozwa na Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Geita, Flavian Kasala.

"Kwa hapa Chato nataka niwahakikishie kwamba miradi yote tuliyopanga na ambayo tumeshaanza kutekeleza, tutaikamilisha hata ile midogo midogo," alisema Rais Samia huku akisisitiza kuwa itakapokamilika atakwenda kuifungua.

Alisema anafahamu juu ya ujenzi wa kivuko cha Hapa Kazi Tu kinachofanya kazi kati ya Chato na Nkome ambacho kimekamilika kwa asilimia 100 na kimegharimu Sh. bilioni 3.1. 


 
Miradi mingine ni ujenzi wa kiwanja cha ndege cha Chato ambao umefikia asilimia 95 kwa gharama ya Sh. bilioni bilioni 58.9 na stendi mpya ya Chato ambayo imegharimu Sh. bilioni 13.2 na ujenzi wake umefikia asilimia 90 na mabasi madogo yameshaanza kuingia. 

Pia alisema amearifiwa kuwa ujenzi wa hospitali ya rufani ya kanda inayojengwa kwa Sh. bilioni 34 unaendelea vizuri na baadhi ya huduma zimeanza kutolewa. 

"Nataka niwaahidi Wanachato, miradi hii itakapokamilika kabisa, nitakuja mwenyewe kuifungua kama ambavyo angefanya Dk. Magufuli kama angekuwapo," alisisitiza Rais Samia. 

Pia alisema serikali imeendelea  kuboresha na kuendeleza huduma za jamii zikiwamo afya, maji, elimu na umeme kama inavyoelekezwa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kama walivyojipanga kutekeleza. 

"Mtakumbuka katika hotuba yangu ya mwanzo kabisa baada ya kuapishwa nilisisitiza kwamba nitayaendeleza mema yote aliyotuachia Hayati Magufuli na kuleta mema mengine mapya," alisema.

Pia alisema wanataka kujenga Tanzania ya kisasa na kuboresha maisha ya Watanzania wote na hayo yote  yatafanikiwa ikiwa, umoja, amani  na mshikamano miongoni mwa Watanzania vitadumishwa. 

Katika hatua nyingine, Rais Samia aliwashukuru viongozi wa dini kwa kuendelea kuliombea taifa na kuliweka mikononi mwa Mwenyezi Mungu.


 

 


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad