Ticker

6/recent/ticker-posts

Vita ya Shilole, Nuh yafika Pabaya

 Habari Kama Hizi Zinapatikana UDAKU SPECIAL App, Download HAPA Bure: Link here>>>KUNA vita ambayo inaendelea kushika kasi kila kukicha kati ya wasanii wawili wa Bongo Fleva ambao waliwahi kuwa wapenzi, Shilole au Shishi Baby dhidi ya Nuh Mziwanda.

Iko hivi; katika kuonesha wamefikia pabaya, Nuh ameweka wazi kuwa ana shauku ya kupigana ngumi na Shilole. Hii ni baada ya kuwepo kwa vita ya kurushiana maneno kwenye mitandao ya kijamii kiasi cha kusababisha wawili hao kutaka pambano la ngumi kati yao.

Nuh ameposti kipande cha video ambacho Shilole alikuwa akifanyiwa mahojiano ambapo anasikika akisema; “Kama unaingia kwenye anga zangu, yule mtoto nitakuja nimkamate nimpige makofi namsubiri…”

Baada ya kuposti video hiyo, Nuh amesema; “Manake hapo kwanza ncheke. Mziwanda mimi au mwingine? Naomba pambano viwanja vipo vingi tu nikuoneshe show Mama Ntilie. Kwanza nna hasira na wewe ulinipiga Leaders Club ukijichanganya tu, nakufumua vibaya sana…”
STORI; SIFAEL PAUL, DAR

HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

________________________________

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments