Wananchi Waomba ijengwe Sanamu ya JPM Ijengwe Chato

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Waomba ijengwe sanamu ya JPM
WANANCHI wilayani Chato mkoani Geita, wameiomba serikali kuwajengea sanamu la aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, hayati Dk. John Magufuli.

Wananchi hao walitoa ombi hilo jana, wakati wa hafla ya kumbukizi ya kifo cha hayati Dk. Magufuli katika uwanja wa Magufuli, uliopo mjini Chato.

Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Wilaya ya Chato, Samuel Bigambo, alisema wanaamini uwepo wa sanamu la kiongozi huyo shupavu litaweka alama isiyofutika kwa vizazi vijavyo.

“Sisi wananchi wa Chato, tulikuwa tunaomba kwanza mkoa, tulishaomba na michakato inaendelea na tunaamini Rais wetu Samia Suluhu Hassan analifanyia kazi.


“La pili ambalo tunaomba, tujengewe sanamu la hayatiDk. Magufuli, liwekwe mahala fulani kama sio pale njia panda ya kwenda mjini kati, basi hata kwenye uwanja wake hapa kuwepo na sanamu.

“ Ikiwekwa sanamu, tutakapokuwa tunapita tunamuona na hata vizazi vitakavyokuja baada yetu, vifike vione kwamba huyu ndiye hayati John Pombe Magufuli, aliyefanya mambo makubwa Tanzania,” alisema.

Naye mkazi wa Kata ya Muungano (Kata ya Magufuli), Esther Kilole, alisema sanamu la hayati Dk.Magufuli likijengwa kwenye mtaa na kata aliyokuwa anaishi, itakuwa ni alama ya kudumu.


“Mimi napendekeza kwamba, sanamu lake lijengwe pale Muungano njia panda, kwani ndiyo katikati ya mji wa Chato, itapendeza sana itakapojengwa pale katikati ya mji wa Chato,” alisema.

Kwa upande wake, Mzee Peter Mwebea, alisema mbali na kujengewa sanamu la hayati Dk. Magufuli wananchi wa Chato wanafarijika kuona kiongozi huyo Taifa linaendelea kumkumbuka.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad