Ticker

6/recent/ticker-posts

Maskini Steve Nyerere Afunguka Haya Baada ya Mwanamuziki RUBY Kutangaza Kuwa Anatamani Afe

 Habari Kama Hizi Zinapatikana UDAKU SPECIAL App, Download HAPA Bure: Link here>>>


Steve Nyerere ameandika haya Kwenda Kwa Ruby:

"Dada Yangu Na Mdogo wangu pia.,(...Ruby) Kwenye Maisha Kila Binadamu Anayo anayo Pitia Kwenye Maisha , Ruby Tunaposema Wanamziki sio waimbaji ,kwangu kuna waimbaji Na wanamziki ,Wewe ni Mwanamziki na Mungu Amekubariki sana una uwezo kubwa sana na kipaji cha kutosha.,

Ruby Usimkaribishe Shetani Kwenye Maisha yako, Natambua una family 👪 Ambayo jicho lote kwako pamoja na mashabiki wako, .,

Mtoto wako ni furaha yako, na ndio kila kitu kwako , Mtoto wako anakutegemea kutimiza malengo yake ,..

Kioo hutuonesha taswira halisi lakini bado hakiwezi kuonesha maumivu yetu,..

Suluhisho la matatizo ni Mungu kupitia watu , Ruby muombe sana Mungu akupe watu sahihi kwenye Maisha.,.

Mungu Anasema,
Niamini nami nitakuongoza na kukuelekeza Kwenye Mipango niliyo nayo juu ya Maisha yako.,.,

Ruby hakuna kukata Tamaa,..Umri wako kipaji chako ni miujiza Tosha unayotakiwa kujipanga kuifanya ,kwa Tanzania 🇹🇿 ya leo mwanamke anayejua kuimba mpaka ukasema sio mwanamziki wa Watanzania ni wewe.,

Ruby yapo mambo unatakiwa kubadilika sana kwenye Maisha , Embu fanya kazi heshimu kazi yako jitume weka akili yako kwenye kuchapa kazi badilisha mfumo mzima wa Maisha yako Tabia yako ,Na penda sana kusikiliza ushauri ,Nidhamu iwe ndio kipaumbele kwenye Maisha yako naimani wakati wa Mungu ndio wakati sahihi kwako.,

Tanzania 🇹🇿 Hiii Hakuna Na bado Hajatokea Mwanamziki wa Kike Mwenye Uwezo kama Wako Ruby anza kujitambua wewe ni Mama wewe hadhina katika mziki.,.,.....

Mungu anasema,..

Nipo karibu

Napigana vita yako

Una thamani

Wewe ni hadhina yangu.,

Una thamani.,.

Ruby don't give up....

MSTAFU KASEMA"

HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

________________________________

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments